Goli la ushindi lililofungwa katika
dakika za mwisho na Anthony Martial, limeendelea kuiweka Manchester
United katika nafasi ya pili ya Ligi Kuu ya Uingereza wakati
wakiifunga Tottenham katika dimba la Old Trafford.
Kuingizwa kwa Martial katika dakika
ya 70 kuchukua nafasi ya Marcus Rashford hakukuwafurahisha mashabiki
wa Manchester United, lakini kocha Jose Mourinho alionekana alikuwa
sahihi baada ya kufunga goli.
Mshambuliaji Mfaransa Anthony Martial akiifungia Man Utd goli pekee katika mchezo huo
Katika mchezo mwingine Leroy Sane
amewasaidia vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza kuibuka na ushindi wa
magoli 3-2 dhidi ya West Brom, lakini kocha Pep Guardiola amewaona
wachezaji wake kuwa wanapaswa kuwa makini katika kupachika magoli.
Katika mchezo huo City walimiliki
mpira kwa asilimia 78 na kutengeneza nafasi 15 za kufunga, huku David
Silva akikosa nafasi mbili za kufunga magoli, wakati naye Kevin de
Bruyne shuti lake likilenga nyavu kwa pembeni.
Leroy Sane akifunga goli la kwanza Manchester City katika mchezo wao dhidi ya West Brom




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni