.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 18 Oktoba 2017

LIVERPOOL YACHARUKA LIGI YA MABINGWA ULAYA NA KUICHAKAZA NK MARBORI

Baada ya kutoka sare tasa na Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza safu ya ushambuliaji ya Liverpool imezinduka katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuifunga NK Marbori kwa magoli 7-0.

Katika mchezo huo Roberto Fermino na Mohamed Salah wote walifunga magoli mawili wakati Liverpool ikipata ushindi mkubwa wa ugenini, huku wakiutawala vilivyo mchezo huo wa kundi E.

Magoli mengine ya Liverpool yalifungwa na Philippe Coutinho, Alex Oxlade-Chamberlain pamoja na Trent Alexander-Arnold ambaye alifunga goli la saba katika dakika ya 90 ya mchezo huo.
    Roberto Fermino akiangali mpira wa kichwa alioupiga ukimshinda kipa na kujaa wavuni
  Mohamed Salah akifunga goli huku Roberto Fermino naye akiwa amejipanga kuuwania mpira huo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni