.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 18 Oktoba 2017

KOCHA PEP GUARDIOLA AJITAPA BAADA YA KUIFUNGA NAPOLI

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, anahisi ushindi wa magoli 2-1 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli ulikuwa umetokana kiwango bora cha timu yake dhidi ya timu bora aliyowahi kukutana nayo.

Katika mchezo huo ulioshuhudia safu mbili hatari katika ushambuliaji Ulaya zikichuana, walikuwa ni Raheem Sterling na Gabriel Jesus waliochangia kuipatia Manchester City kupata ushindi kwa kufunga magoli hayo mawili.

Napoli inayoongoza ligi ya Serie A kwa kushinda michezo yote nane katika msimu huu, walipatiwa penati mbili katika mchezo huo moja iliyopigwa na Dries Mertens ikiokolewa na nyingine ikifungwa na Amadou Diawara.
    Raheem Sterling akifunga goli la kwanza la Manchester City katika mchezo huo
                           Mbrazil Gabriel Jesus akitumbukiza goli la pili la Manchester City

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni