.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 19 Oktoba 2017

PARIS SAINT-GERMAIN YASHINDA KIRAHISI MCHEZO WAKE NA ANDERLECHT

Paris Saint-Germain ilihitaji chini ya dakika tatu kuonyesha mamlaka yake katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Anderlecht.

Kylian Mbappe alifunga goli la kwanza akiwa kwenye eneo gumu kufunga na kisha baadaye akamtengenezea Edinson Cavani goli la kichwa alilofunga kiulaini.

Baada ya mapumziko Neymar, alifunga goli kwa mpira wa adhabu ulioipenya ukuta wa ulinzi na kumshinda kipa Matz Sels na kisha baadaye Angel Di Maria akafunga goli la nne.
                                          Mshambuliaji kinda wa PSG Kylian Mbappe akifunga goli 
       Mchezaji wa zamani wa Manchester United Angel Di Maria akiifungia PSG goli la nne

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni