Kanisa linalohamasisha waumini wake
kunywa pombe, kuwabatiza kwa kutumia pombe aina ya Whisky na
kuwakaribishwa walevi limekuwa na umaarufu zaidi nchini Afrika
Kusini.
Askofu wa kanisa hilo la pombe
rukhsa hadi kanisani, Tsietsi Makiti amekuwa akibariki pombe wakati
wa ibada kila wiki huko Evaton, Afrika Kusini.
Askofu Makiti ni kiongozi wa kanisa
hilo la Gabola lenye waumini 500 ambao ni wanywaji wa pombe ambao
hufanya ibada yao siku ya jumapili maenao mbalimbali ya Jiji la
Johannesburg.
Askofu Tsietsi Makiti akiwa na kopo kubwa la Castle akilibariki kanisani
Mmoja wa waumini wa kanisa akibatizwa na Askofu Tsietsi Makiti kwa pombe ya kwenye kopo aliyoichagua
Waumini wa kanisa wakiwa wameshikilia vinywaji vyao vikiombewa na kutakaswa na askofu Tsietsi Makiti
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni