Kocha wa Italia Giampiero Ventura
amesema kuwa kikosi chake kitahitaji kuongeza kiwango chake katika
mchezo wa marudio na Sweden ili kuepuka kukosa michuano ya kombe la
dunia kwa mara ya kwanza tangu 1958.
Timu ya taifa ya Sweden imeshinda
mchezo wa kwanza kwa goli 1-0 katika dimba la Friends Arena, goli
hilo pekee likifungwa na Jakob Johansson akiachia shuti la umbali wa
yadi 20 kufuatia krosi ya Daniele de Rossi iliyogongwa.
Italia ilionekana kuimarika katika
kipindi cha pili cha mchezo huo lakini kiwango hicho walichoonyesha
hakikuisaidia kusawazisha goli hilo, licha ya Matteo Darmian
kukaribia kufunga lakini shuti lake likagonga mwamba.
Mpira uliopigwa na Jakob Johansson ukiwa umetinga wavuni mwa lango la Italia
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni