Mshambuliaji wa PSG Neymar ametokwa
machozi baada ya kocha wa timu ya taifa ya Brazil Tite kumtetea baada
ya kuibuka na ushindi Ijumaa dhidi ya Japan.
Gazeti moja la Ufarasa hivi karibuni
liliandika uhusiano baina ya bosi wa PSG Unai Emery na Neymar
umetibuka hivi karibuni, ikiwa ni miezi michache anunuliwe kwa kitita
cha paundi milioni 198, akitokea Barcelona.
Hata hivyo, Neymar amekuwa
amekanusha vikali madai hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika baada ya kuishinda Japani kwa magoli 3-1 huko Lille.
Kocha Tite akimshika kichwa Neymar kumbembeleza baada ya kuangua kilio
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni