Dereva wa mbio za magari za
Langlanga Lewis Hamilton amesema amechukizwa na habari ya watumishi
wa timu ya Mercedes kuibiwa kwa mtutu Jijini Sao Paul Brazil jana
usiku.
Gari la watumishi wa Mercedes
lilizimamishwa kwenye barabara na waporaji wenye silaha hata hivyo
hakuna mtu aliyedhuriwa katika tukio hilo.
Hamilton amesema kuwa katika tukio
hilo risasi zilifyatuliwa na watumishi hao wa Marcedes waloelekezewa
bastola vichwani mwao, na kuongeza kuwa inaudhi mno kusikia haya.
Hamilton amesema kwamba matukio ya
uporaji Sao Poul nchini Brazil hutokea kila mwaka na kuutaka uaongozi
wa F1 kuimarisha zaidi ulinzi na wasitafute sababu za kujitetea.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni