Mabingwa mara nne wa kombe la dunia
Italia wameshindwa kufuzu fainali za kombe la dunia kwa mara ya
kwanza tangu mwaka 1958 baada ya kushindwa kuifunga Sweden katika
mchezo wa marudio.
Hii inaamaana Italia maarufu kama
Azzurri hawatokuwepo katika michuano hiyo ya soko ya dunia nchini
Urusi mwakani, ikiwa ni mara ya pili kujikuta kuwa katika hali hiyo
katika historia ya michuano hiyo tangu mwaka 1930.
Goli la kiungo Jakob Johansson la
shuti lililogongwa na kumpoteza mahesabu kipa katika mchezo wa kwanza
lilitosha kuifungasha virago Italia baada ya jana kutoka sare tasa
huko Milan katika dimba la San Siro.
Wachezaji wa Sweden wakishangilia kufanikiwa kufuzu fainali za kombe la dunia
Kipa wa Italia Gianluigi Buffon akipungia mashabiki kwa huzuni kuwaaga baada ya kutangaza kustaafu soka la kimataifa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni