Maelfu ya wananchi w Iran wamelala
nje usiku wa jana katika hali ya baridi kali baada ya kukumbwa na
tetemeko lililobomoa majengo na kusababisha vifo magharibi mwa nchi
hiyo.
Serikali inahaha kupata msaada kwa
maeneo yaliyoathirika mno katika mkoa wenye milima wa Kermanshah,
ambao mamia ya nyumba zimeathirika.
Zaidi ya watu 400 wamekufa na zaidi
ya watu 7,000 wamejeruhiwa wakati tetemeko lilipolikumba eneo la
mpaka wa Iran na Irak jumapili.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni