.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 26 Novemba 2017

KOCHA JURGEN KLOPP AKASIRISHWA KUNYIMWA KUFANYA 'SUB'

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amekasirishwa mno na kikosi chake kushindwa kufanya mabadiliko kabla ya mchezaji aliyetokea benchi Willian kusawazisha na kuisaidia Chelsea kutoa sare ya goli 1-1 katika dimba la Anfield.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Uingereza Liverpool ilikuwa ya kwanza kupata goli lililofungwa na mchezaji wazamani wa Chelsea Mohamed Salah kwa shuti la karibu lakini Willian alifuta ndoto za ushindi kwa kusawazisha goli.

Goli hilo la Mmisri Mohamed Salah ni la 10 katika michezo 13 ya Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu huu, akiwa ameanza vyema kibarua chake tangu ajiunge na Liverpool.
        Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah akiifunga timu yake ya zamani goli
    Mpira uliopigwa na Mbrazil Willian ukimshinda kipa wa Liverpool na kujaa wavuni

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni