Kocha wa Manchester City Pep
Guardiola amesema kuwa kikosi chake kimefanya vyema baada ya
kupambana kutokea nyuma kufungwa goli hadi kuibuka na ushindi wa
magoli 2-1 dhidi ya Huddersfield.
Vinara hao wa Ligi Kuu ya Uingereza
wamefikia rekodi ya klabu hiyo ya mwaka 2015 kwa kupata ushindi wa 11
mfululizo licha ya kuanza kwa kujifunga goli kupitia kwa Nicolas
Otamendi.
Alikuwa Sergio Aguero
aliyeisawazishia goli Manchester City kwa penati katika kipindi cha
pili na kisha baadaye Raheem Sterling aliipatia goli la ushindi
katika dakika za mwisho zikiwa zimebakia dakika sita.
Kipa Jonas Loss akiwa amepotezwa mahesabu na Sergio Aguero
Raheem Sterling akiwa anangojea mpira uliogonga mbamba na kumpatia nafasi ya kufunga
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni