Goli la dakika za mwisho la Lars
Stindl limewasaidia mabigwa wa dunia Ujerumani kuendeleza rekodi ya
kutofungwa michezo 21 baada ya kutoka sare ya magoli 2-2 na Ufaransa.
Katika mchezo huo wa kirafiki wa
kimataifa kazi nzuri ya Anthony Martial ilisaidia kupatikana goli la
kwanza la Ufaransa lililofungwa na Alexandre Lacazette.
Timo Werner alitumbukiza kimiani
pande la Mesut Ozil kabla ya Lacazette tena kufunga goli zuri na
kufanya matokeo kuwa 2-1.
Anthony Martial akitoa pande la kufunga goli kwa Alexandre Lacazette
Timo Werner akitumbukiza mpira wavuni uliomshinda kipa wa Ufaransa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni