Sergio Aguero amepelekwa hospitali
baada ya kuzimia katika chumba cha kubadilishia nguo kipindi cha
mapumziko katika mchezo ambao Argentina ilifungwa magoli 4-2 na
Nigeria.
Mshambuliaji huyo wa Manchester City
alifunga goli la pili na kufanya Argentina kuongoza kwa magoli 2-0
baada ya Banega kufunga goli la kwanza.
Aguero alipelekwa hospitali na
baadaye kuruhusiwa, hata hivyo kipindi cha pili Nigeria walirekebisha
makosa na kufunga magoli kupitia kwa Iheanacho, Iwobi mawili na Idowu
moja.
Sergio Aguero akifunga goli la pili la Argentina kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza
Kelechi Iheanacho akinyoosha vidole juu kumshukuru Mungu baada ya kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni