.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 19 Novemba 2017

MANCHESTER CITY YAENDELEZA MAKALI LIGI KUU YA UINGEREZA

Manchester City imeendeleza makali yake katika Ligi Kuu ya Uingereza na kuifunga Leicester City magoli 2-1 na kuendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi nane.

Manchester City walipata goli lao la kwanza kupitia kwa Gabriel Jesus kabla ya mapumziko akinasa pasi ya David Silva na kisha Kevin de Bruyne akafunga la pili katika kipindi cha pili.
  Gabriel Jesus akiwa ametumbukiza wavuni mpira na kufunga goli la kwanza la Manchester City
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema magoli mawili yaliyofungwa na Mohamed Salah yamekisaidia kikosi chake kuwa na siku nzuri dhidi ya Southampton.

Katika mchezo huo ambao Liverpool iliibuka na ushindi wa magoli 3-0 ukiwa ni watatu mfululizo kuupata katika Ligi Kuu ya Uingereza, Philippe Coutinho naye alitikisa nyavu.
  Kipa wa Southampton akiruka bila ya mafanikio kuufuata mpira uliopigwa na Mohamed Salah

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni