Morocco imefuzu kutinga fainali za
kombe la dunia 2018 baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi
ya Ivory Coast ambao wameshinda kwa mara ya nne mfululizo kutinga
fainali hizo.
Magoli kutoka kwa beki Nabil Dirar
na Medhi Benatia katika mchezo uliochezwa Abidjan yaliwahakikishia
Morocco kumaliza washindi katika kundi C.
Morocco ilikuwa inahitaji sare tu
kumaliza ikiongoza kundi hilo mbele ya Ivory Coast iliyopaswa
kushinda ili kukata tiketi ya kwenda Urusi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni