Mabingwa wa Afrika Cameroon
wamelazisha sare ya magoli 2-2 dhidi ya Zambia katika mchezo wao wa
mwisho wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia, ikiokolewa na
Yaya Banana.
Timu zote mbili zilishuka dimbani
zikidhamiria kumaliza kampeni zao kwa ushindi, licha ya kushindwa
kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 nchini Urusi.
Alikuwa Patson Daka aliyeifanya
Zambia iongoze katika dakika ya 26, akinasa pande la Fashion Sakala
na kutikisa nyavu, lakini dakika tano baadaye Andre Zambo Anguissa
alisawazisha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni