Tunisia imekata tiketi ya kucheza
fainali za kombe la dunia baada ya kutoka na pointi moja dhidi ya
majirani zao Libya hapo jana katika mchezo ulioishia kwa sare ya 0-0.
Tunisia imemaliza ikiwa na pointi 14
katika kundi A, ikiwa mbele ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
iliyoshinda magoli 3-1 dhidi ya Guinea Jijini Kinshasa.
Tunisia ambayo haikufungwa
imeshashiriki mara nne katika fainali za kombe la dunia na ilikuwa
timu ya kwanza Afrika kushinda mchezo katika michuano hiyo mwaka
1978.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni