Katika mahafali hayo zaidi ya wanachuo 1,443 waliochukua mafunzo ya Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu, (BAED), Shahada ya Elimu ya Sayansi na Elimu, (Bsc) na Shahada ya Elimu (BED), pamoja na wahitimu waliojiendeleza (Post graduate), walitunukiwa shahada ya kwanza, ambapo mwanachuo Dadi Omary Safari, alipewa tuzo ya kuwa mwanachuo bora zaidi kitaaluma.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akimpongeza mmoja wa wahitimu wa Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu, (BAED) Bi Amisa Hassan. |
Furaha ya kuhitimu na kutunukiwa shahada.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, akisoma hotuba yake.
Dkt. Kikwete, akipitia ratiba ya mahafali hayo.
Dkt. Kikwete akitangaza kuwatunuku shahada baadhi ya wanachuo hao. |
Dkt. Kikwete, akiteta jambo na Profesa Mukandala.
Dkt. Kikwete, akiipitia tuzo ya mwanachuo bora kitaaluma Dadi Emmanuel Safari kabla ya kumkabidhi.
Mwanachuo bora kitaaluma Dadi Emmanuel Safari akiwa na tuzo yake.
Dkt. Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa wahitimu, Amisa Hassan, na baba mdogo wa muhitimu huyo, Khalfan Said.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni