Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Kizumba kata ya Laela Wilayani Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiongea na wananchi wa Kijiji cha Zimba kwa lengo la kujitambulisha kwa wananchi hao wa bonde la ziwa Rukwa kata ya Mtowisa, Wilaya ya Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameiagiza kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga kuhakikisha wanashirikiana na Halmashauri kupunguza idadi ya mifugo iliyopo kwenye halmashauri hiyo ili kudhibiti utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja na hifadhi za misitu na kuliokoa ziwa Rukwa.
Amesema kuwa shughuli hizo za ufugaji karibu na vyanzo vya maji ndizo zinazopelekea kujaa kwa tope katika ziwa Rukwa, ziwa linaloasisi jina la Mkoa huo na kuongeza kuwa serikali haipo tayari kuona ziwa hilo likipotea na kusisitiza kuhifadhiwa kwa namna yoyote ile ikiwemo kupiga marufuku kufanbya shughuli za ufugaji kwenye vyanzo vya maji.
“Nashkuru kwamba zoezi la kupiga chapa linaendelea ila baada ya kumaliza zoezi hilo muanze kwenda boma kwa boma muhakikishe kwamba animal Unit “idadi ya mfugo kwa eneo” inazingatiwa, mtu ashauriwe kupunguza mifugo yake au ahame akatafute mahali pengine, kwasababu hatuwezi kujaza mifugo kwenye bonde la ziwa Rukwa halafu ziwa likafutika, serikali haitakubali.” Alibainisha.
Ameyasema hayo baada ya kusomewa taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga katika Ziara yake ya siku mbili yenye lengo la kutembelea miradi mbalimbali, kujitambulisha kwa watumishi pamoja na kuongea na makundi mbalimbali ya wananchi katika halmashauri hiyo.
Katika taarifa hiyo ilionesha kuwa idadi ya wanyama iliyopo katika bonde hilo ni 143,346 huku idadi inayotakiwa ni 36,666 huku ikionesha kuongezeka mara tatu zaidi ya mahitaji ya uwepo wa Wanyama hao katika bonde hilo.
Katika kulisisitiza hilo Mh. Wangabo amewatahadharisha wananchi kufuga kisasa kwa kuwa na mifugo michache yenye kuleta tija huku ikizingati uhitaji wa ardhi kwaajili ya kilimo na shughuli nyingine za kibinaadamu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa skimu ya umwagiliaji Kijiji cha Ng’ongo, kata ya Mtowisa Wilayani Sumbawanga, Justin Amon amesema kuwa wafugaji wamekuwa wengi katika bonde hilo hasa katika skimu yao hiyo na kuwasababishia hasara pale wanapopeleka mifugo yao kwaajili ya malisho.
“Kama taarifa ilivyosomwa wafugaji wapo wengi ambao wamegeuza eneo hili kuwa sehemu ya machungio, tunapojaribu kuwafuatilia wanatushishia na mawe, fimbo, sime na mapanga na wapo tayari kupambana kwa lolote litakalotokea, na kesi zipo mahakamani lakini tunaambiwa hatujakamilisha vigezo, hivyo tunashindwa na kushindwa kujua kwamba tunasaidiwaje na serikali yetu, wafugaji wanatunyanyasa sana,” Alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameziagiza halmashauri nne za mkoa huo kushirikiana na Shirika la viwanda vidogo nchini SIDO kuhakikisha wanakuwa na viwanda vipya 25 hadi kufikia Disemba mwaka 2018 ili kutimiza agizo la serikali la kuwa na viwanda 100 vipya kwa kila Mkoa.
Amesema kuwa SIDO ndio msaada mkubwa wa kuhakikisha kuwa ndoto hii inatimia kwani shirikia hilo limejaa wataalamu lakini pia hutoa mafunzo ya viwanda vidogo na vya kati kwa wajasiliamali hivyo hawana budi kuwa nao karibu.
“Serikali imekwishaagiza tuwe na viwanda 100 hadi kufikia Disemba mwaka 2018 na kwa mahisabu ya haraka mkoa una Halmashauri nne, 100 ukigawa kwa nne ni 25, kwahiyo hadi kufikia Disemba 2018 kila Halmashauri iwe na viwanda hivyo vipya, na msaada upo kuna SIDO hapo ambao wataalamu wamejaa na wanatoa mafunzo kila siku ya viwanda vidogo na vya kati watawasadidia na mimi nitalisismamia,” Alisema
Ameyasema hayo baada ya kupokea malalamiko ya diwani wa kata ya Mtowisa Mh. Edgar Malini. alipomkabidhi Mh. Wangabo Skafu iliyotengenezwa na kilichokuwa kiwanda cha nguo katika kata hiyo ambacho kilifungwa miaka zaidi ya 30 na kubaki majengo.
Mh. Edgar Malini alisema kuwa kiwanda hicho kilifunguliwa na Aliyekuwa Waziri Mkuu Mh. Rashid mfaume Kawawa lakini kwa sasa uzalishaji wake umekwama kwani pamba haipatikani kwenye maeneo yao na hivyo kuwa na mazingira magumu ya uzalishaji wa nguo katika kiwanda hicho.
Kwa sasa Mkoa wa Rukwa una jumla ya viwanda 950 huku kukiwa na kiwanda kikubwa kimoja, viwanda vya kati 2 na viwanda vidogo 947.

Skafu - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akivishwa Skafu na Diwani wa kata ya Mtowisa Mh. Edgar Malini, Skafu hiyo iliyotengenezwa na kilichokuwa kiwanda cha nguo kata ya Mtowisa kilichokufa na kubaki majengo tu.
Kijiji cha Zimba - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akisalimia na Mzee Gabrieli Joseph, miongoni mwa wazee wa kijiji hicho chenye kiwanda cha kukamulia Alizeti kinachoendeshwa na Mwalimu wa Shule. wakati alipokwenda kujitambulisha kwa wananchi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni