Mchezaji soka wa Brazil Robinho
amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela kwa kuhusika katika tukio la
ubakaji lililohusisha kundi la wanaume huko Milan nchini Italia mnamo
mwaka 2013.
Mahakama ya nchini Italia imetoa
huku kwa mchezaji huyo mwenye miaka 33 na wenzake watano raia wa
Brazil kwa kumbaka mwanamke raia wa Albainia aliyekuwa na miaka 22
wakati huo baada ya kumlewesha kwenye klabu ya usiku.
Mshambuliaji huyo aliondoka AC Milan
mwaka 2015 baada ya kuitumikia kwa miaka mitano na wakati hukumu hiyo
ikitolewa hakuwepo Mahakamani na alikanusha shtaka hilo kupitia kwa
wakili wake.
Hata hivyo Robinho hataanza kutumikia kifungo hicho kwanza hadi hapo rufaa yake ya hukumu hiyo itakaposikilizwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni