Ligi ya wanawake inatarajia kuanza Jumapili Novemba 26, 2017 kwenye vituo viwili vya Dar Es Salaam na Arusha ambapo kundi A litakuwa Dar es Salaam likitumia Uwanja wa Karume wakati kundi B litakuwa Arusha likitumia Uwanja wa General Tyre.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa uzinduzi wa Ligi Kuu soka ya Wanawake, imefahamika.
Mbali ya Dk. Mwakyembe, wageni wengine wanaotarajiwa kuwa katika uzinduzi huo ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo; Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred pamoja na viongozi wengine wakiwamo Wakuu wa Wilaya mbalimbali za Arusha na mikoa ya jirani.
Kundi A lina timu za Mlandizi Queens ya Pwani, JKT Queens ya Dar es Salaam, Fair Play ya Tanga, Simba Queens ya Dar es Salaam, Ever Green Queens ya Dar es Salaam na Mburahati Queens ya Dar Es Salaam.
Kundi B lenyewe linajumuisha timu za Marsh FC ya Mwanza, Kigoma Sisters ya Kigoma, Panama FC ya Iringa, Baobab Queens ya Dodoma, Alliance Queens ya Mwanza na Majengo Queens ya Singida.
Ufunguzi rasmi wa ligi hiyo utafanyika mkoani Arusha Jumapili Novemba 26, 2017 na mchezo wa ufunguzi utakuwa kati ya Panama FC itakayocheza na Alliance Queens mchezo utakaotanguliwa na hafla ya ufunguzi.
Katika siku hiyo kituo cha Dar Es Salaam kinachotumia Uwanja wa Karume nako kutakuwa na mchezo mmoja utakaowakutanisha Mlandizi Queens dhidi ya JKT Queens.
UAMUZI WA KAMATI KUHUSU USAJILI LIGI YA WANAWAKE
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyokutana Novemba 22, 2017, katika ofisi za TFF Karume, pamoja na mambo mengine ilijadili shauri la mapingamizi mbalimbali yaliyowekwa na timu za Ligi ya Wanawake.
Timu ya Mburahati Queens iliweka pingamizi kwa mchezaji Ever Kombo ikipinga timu ya Baobab kumtumia kwa kuwa hakulipiwa ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake.
Kamati imeiruhusu timu ya Baobab kumtumia mchezaji huyo baada ya Mburahati Queens kuondoa pingamizi hilo.
Aidha Kamati imeiruhusu timu ya Fair Play ya Tanga kumtumia mchezaji Anastazia Mmwacha baada ya timu ya Mburahati Queens kuondoa pingamizi iliyomuwekea kwa kutolipiwa ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake.
Kamati imeiruhusu timu ya Panama kumtumia mchezaji Sabina Mbuta aliyewekewa pingamizi na Mburahati Queens kwa kutolipiwa ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake,Panama wameruhusiwa kumtumia baada ya kulipa ada hiyo ya shilingi laki moja(100,000).
Timu ya Marsh Academy imeruhusiwa kuwatumia wachezaji Asfaty Kasindo,Janeth Simba ,Rose Mpoma na Arafa Ramadhan wa Mlandizi Queens,Monica Conrad,Christer J Bahera na Niwael Makuluta wa Mburahati Queens, Neema Kiniga wa Kigoma Sisters baada ya kukubali kuzilipa timu zao ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake na timu hizo kukubali kuondoa pingamizi.
Nayo, timu ya JKT Queens imeruhusiwa kuwatumia wachezaji Najiat Abassi,Fumu Ally,Hamisa Athuman wa Ever Green Queens,Fatuma Makusanya na Elizabeth Kadonya wa Mburahati Queens baada ya timu zao kuondoa mapingamizi waliyoweka kwa wachezaji hao kutolipiwa ada ya uhamisho.
Timu ya Simba Queens imezuiwa kuwatumia wachezaji Zainab Rashid wa Ever Green Queens, Grace T Mbelayi, Jackline Kulsanga, Dinna Omary wa Mlandizi Queens, na Halima Hamdani Mchen wa Kigoma Sisters mpaka pale watakapolipa ada ya uhamisho wa shilingi laki moja (100,000) kwa kila mchezaji kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya wanawake.
Mapingamizi yaliyowekwa na timu ya Makongo High School kwa timu mbalimbali ikipinga timu hizo kuwatumia wachezaji wake bila kulipa ada,mapingamizi hayo yametupwa baada ya timu hiyo kushindwa kufika kutetea hoja za mapingamizi hayo.
Timu ya Marsh Academy ya Mwanza imeruhusiwa kuwatumia wachezaji Zainab Hassan Kienje na Silva Daud waliowekewa pingamizi na timu ya Kigoma Sisters ambayo ilishindwa kufika kwenye kikao cha kujadili pingamizi lake.
Wachezaji Asia Juma,Betista Othuman Abdala na Josephine Julius Nyirenda wameruhusiwa kucheza timu ya Baobab baada ya timu ya Kigoma Sisters iliyowawekea pingamizi kuamua kuyaondoa mapingamizi hayo.
KARIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA GAMA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama.
Kutokana na msiba huo, Rais Karia ametua salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Kadhalika Rais Karia ametuma salamu za salamu rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Ruvuma (FARU), Golden Sanga pamoja na Mwenyekiti wa Majimaji ya Songea, Steven Ngonyani na wanafamilia wote wa mpira wa miguu na wananchi wote wa mjini Songea.
“Songea ina historia ya mpira na akina Gama ni chachu ya maendeleo ya mpira wa miguu Songea. Tumepoteza hazina nyingine, lakini niombe tu familia ya Gama, ndugu, jamaa na marafiki kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwao,” amesema.
“Nawapa pole nyingi sana na kupitia viongozi wa FARU, Majimaji, Mlale JKT na wanafamilia wengine wa soka katika Mkoa wa Ruvuma, naomba mfikishe salamu zangu za pole kwa familia ya marehemu,” amesema Rais Karia.
Rais Karia amesema anamkumbuka Gama kwa uhodari wake katika nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwemo ukuu wa wilaya, mkoa na ubunge kwani alifanya kazi kwa kujiamini na kupenda kupigania maendeleo hususani mpira wa miguu bila kuchoka.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni