Cristiano Ronaldo amefunga goli la
ushindi katika dakika za mwisho na kuifanya Real Madrid kusogea
pointi saba nyuma ya vinara wa ligi ya La Liga Barcelona baada ya
kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Malaga.
Ronaldo alifunga goli hilo baada ya
kukutana na mpira uliookolewa na kurudi, ikiwa ni baada ya kukosa
penati katika dakika ya 76, iliyookolewa na kipa wa Malaga Roberto
Jimenez.
Katika mchezo huo Real iliongoza
mara mbili kufunga lakini ikajikuta magoli yao yakirejeshwa mara
mbili na wageni, hii ni baada ya Karim Benzema kufunga goli la kwanza
na Casemiro la pili.
Timu hiyo inayonalewa na kocha
Mfaransa Zinedine Zidane imejikuta ikishushwa hadi katika nafasi ya
nne katika msimamo wa La Liga kwa tofauti ya magoli baada ya Atletico
Madrid kuipiga Levante 5-0.
Mshambuliaji nyota duniani Cristiano Ronaldo akifunga goli la ushindi la Real Madrid dhidi Malaga
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni