Kocha Antonio Conte amesema ni
kukosa bahati tu kulioifanya timu yake wa Chelsea kuwa pointi 13
nyuma ya vinara wa ligi Manchester City baada ya kuifunga Brighton
2-0.
Chelsea imepata ushindi wa sita
mfululizo katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya jana kusakata
kandanda safi na kupata magoli hayo kupitia kwa Alvaro Morata na
Marcos Alonso.
Alvaro Morata akifunga kwa mpira wa kichwa goli la kwanza la Chelsea
Shuti la Jesse Lingard limeinyima
Burnley kupata ushindi katika dimba la Old Trafford na kutoka sare ya
magoli 2-2 matokeo ambayo yanafifisha matumaini ya kukimbiza ubingwa.
Katika mchezo huo Ashley Barnes
aliwafungia wageni goli la kwanza na kisha baadaye Steven Defour
akafunga goli la pili na kufanya hadi mapumziko matokeo kuwa 2-0.
Jesse Lingard akiachia shuti na kuisaidia Manchester United kulazimisha sare dhidi ya Burnley




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni