Betri kubwa kabisa duniani aina ya
lithium imeanza kusambaza umeme kuingiza katika gridi ya umeme kusini
mwa Australia.
Betri hiyo inayozalisha umeme wa
Megawati 100, imetengenezwa na kampuni ya Tesla, imezinduliwa rasmi
leo, licha ya kuanza kusambaza umeme tangu jana,
Hali ya joto kali imechangia
kuongezeka kwa mahitaji ya umeme kusini mwa Australia na Bosi wa
Tesla Elon Musk aliahidi kujenga betri kubwa na kufanikisha kufanya
hivyo ndani ya siku 100.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni