.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 20 Januari 2018

HAZARD ACHARUKA CHELSEA IKIICHAKAZA BRIGHTON

Eden Hazard amerejesha makali yake kwa kufunga magoli mawili na kuisaidia Chelsea kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Brighton.

Eden Hazard alifunga goli la kwanza kwa kumalizia vyema mpira ndani ya eneo la penati kisha kiungo Willian akaongeza la pili kwa umbali wa yadi 18.

Hazard tena akafunga goli la tatu, kisha Victor Moses akafunga goli la nne, na kuifanya Chelsea kufikisha pointi sawa na Mannchester United katika nafasi ya pili.
   Eden Hazard akifunga goli la kwanza katika mchezo huo kwa shuti la ndani ya eneo la penati
Hazard akifunga goli lake la pili huku mchezaji mwenzake Michy Batshuayi akiwa amelala chini akiangalia mpira
                    Victor Moses akikamilisha ushindi mnono kwa kufunga goli la nne la Chelsea 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni