Kocha wa Leicester Claude Puel
amesema uamuzi wa kumtoa kwa kadi nyekundu Ben Chilwell katika mchezo
wa Chelsea ulikuwa wa ghadhabu, na kufanya kikisi chake kitoke sare
badala ya kupata ushindi.
Leicester City waliutawala mpira na
kuumiliki kwa muda mwingi na walikuwa na nafasi nzuri ya kushinda,
lakini mambo yalibadilika baada ya beki Chilwell kupewa kadi ya njano
ya pili.
Beki huyo hakuonewa huruma na refa
Mike Jones katika dakika ya 68 pale alipomuangusha Victor Moses,
ikiwa ni muda mfupi tu tangu amchezee rafu Mbrazil Willian, katika
mchezo huo ulioishia kwa sare tasa.
Kipa wa Leicester City Kasper Schmeichel akipangua kiufundi moja ya mipira iliyoelekezwa katika lango lake
Refa Mike Jones akimpa kadi nyekundu beki Ben Chilwell baada ya kumchezea rafu Victor Moses
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni