Meneja wa Tottenham Mauricio
Ponchettino anaunga mkono Harry Kane kuvunja rekodi ya ufungaji ya
klabu hiyo mara baada ya kufunga magoli mawili katika ushindi mwepesi
wa magoli 4-0 dhidi ya Everton.
Harry Kane alifunga magoli hayo
mawili karibu na lango akimalizi pasi za Son Heung-min na Eric Dier
na kufikisha idadi ya magoli 98 katika Ligi Kuu ya Uingereza akimzidi
Teddy Sheringham kwa goli moja aliyoifungia klabu hiyo.
Katika mchezo huo Son aliyekuwa
kwenye ubora wake alifungua mvua ya magoli akiunganisha wavuni krosi
ya Serge Aurier. Tottenham ilipata goli lake la nne kupitia kwa
Christian Eriksen akinasa pasi ya kisigino ya Dele Alli.
Mshambuliaji Harry Kane akifunga moja ya magoli yake mawili aliyofunga jana
Mshambuliaji raia wa Korea Kusini Son Heung-min akiifungia Tottenham goli la kwanza
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni