Ligi ya Wanawake ya Serengeti
Premier Lite hatua ya nane bora inatarajia kuanza kutimua vumbi
Februari 24, 2018 kwenye viwanja vine.
Mchezo kati ya Kigoma FC na Simba
Queens utakaochezwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika ndio utakuwa
mchezo rasmi wa ufunguzi.
Mechi nyingine zitakazochezwa katika
siku hiyo ya ufunguzi ni Panama watakaokuwa nyumbani Uwanja wa Samora
kucheza na Evergreen,JKT Queens wakicheza dhidi ya Alliance kwenye
uwanja wa Mbweni.
Mechi nyingine ni ile
nitakayowakutanisha Baobab na Mlandizi Queens utakaochezwa kwenye
uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Kabla ya kufika kwenye hatua
hiyo,ligi hiyo inayodhaminiwa na bia ya Serengeti Premier Lite
kinywaji murua na chenye ubora wa juu ilianzia kwenye hatua ya
makundi ikichezwa kwenye Kituo cha Dar Es Salaam kilichotumia Uwanja
wa Karume na Kituo cha Arusha kilichotumia Uwanja wa General Tyre.
CAF YAMTEUA MGOYI KUSIMAMIA MECHI YA
KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRICA KWA VILABU
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani
Africa CAF limemteua Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania TFF Ahmed Mgoyi kuwa Kamishna wa mchezo wa
Kombe la Shirikisho kwa klabu kati ya AFC Leopards ya Kenya na Fosa
Juniors ya Madagascar.
Mchezo huo namba 13 utachezwa nchini
Kenya kati ya Februari 9,10 na 11 mwaka huu.
Kwenye mchezo huo waamuzi wote
wanatoka nchini Somalia ambapo mwamuzi wa kati ni Abdulkadir Artan
Omar,mwamuzi msaidizi namba moja Ali Mohamed Mahad,mwamuzi msaidizi
namba mbili Ahmed Abdullah Farah wakati mwamuzi wa akiba ni Hassan
Mohamed Hagi.
Mgoyi ni miongoni mwa Wajumbe wa
Kamati ya utendaji wa TFF walioteuliwa hivi karibuni kuwa makamishna
wa mechi zinazoandaliwa na CAF kwa mwaka 2018 mpaka mwaka 2020
wengine ni Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura,Amina Karuma na
Sarah Tchao.
Aidha Rais wa TFF Ndugu Wallace
Karia naye mbali ya kuteuliwa kwenye kamati ya mashindano ya fainali
za Africa kwa wachezaji wanaocheza ndani CHAN tayari amechaguliwa
mara mbili kusimamia mechi za CHAN zinazoendelea nchini Morocco.
Alisimamia mechi ya ufunguzi
iliyowakutanisha Wenyeji Morocco na Mauritania Januari 13, 2018 na
mchezo wa pili uliochezwa jana Januari 22, 2018 kati ya Namibia na
Zambia.
CAF YAJA TANZANIA UKAGUZI MFUMO WA
LESENI KWA VILABU
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani
Africa CAF litafanya ukaguzi wa mfumo wa leseni kwa vilabu(Club
Licencing) kwenye upande wa miundo mbinu.
CAF watafanya ukaguzi huo wa
kutembelea na kutazama miundo mbinu ili kuhakikisha mfumo huo
unatekelezeka ipasavyo kwa kuanzia na mtazamo wa vigezo vya miundo
mbinu.
Wakati wa miaka kadhaa ya kuzindua
mfumo huo wa leseni kwa vilabu ni wazi changamoto kubwa kwenye Bara
la Africa imekuwa ni vigezo vya miundo mbinu ambayo kwenye baadhi ya
viwanja vinavyotumika wakati wa mashindano imekuwa ikitoa taswira
isiyo nzuri kwa mashindano ya CAF.
Kwa mwaka huu 2018 wameandaa ukaguzi
kutembelea klabu zote zitakazoshiriki hatua ya makundi kwenye
mashindano ya vilabu ya CAF wakijielekeza kwenye kiwango na ubora wa
viwanja vya kucheza mechi na viwanja walivyochagua kwa mazoezi.
Caf watachagua kundi la wakaguzi
watakaotembelea kwenye klabu za kila mwanachama wake ili kukusanya
ripoti itakayowasilishwa na moja kati ya ripoti hiyo ni miundo mbinu
ya Uwanja,ripoti itakayothibitisha kama uwanja umefikia kwenye
mahitaji ya juu ya kutumika kwa mechi za CAF.
Viwanja ambavyo havitakidhi mahitaji
hayo ya juu hautaidhinishwa kutumika kwa mashindano na hautatumika
kwa mchezo wowote wa hatua hiyo ya makundi kwa mashindano ya klabu
kwa mwaka huu 2018.
UKAGUZI WA VIWANJA KOMBE LA
SHIRIKISHO LA AZAM VITATU KUTOTUMIKA HATUA YA RAUNDI YA TATU
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania TFF limefanya ukaguzi wa viwanja vinavyotumika kwa kombe la
Shirikisho na kuzuia viwanja vitatu kutumika kwa mechi zinazofuata za
hatua ya raundi ya tatu.
Viwanja ambavyo havitaweza kutumika
kwa raundi hiyo ya tatu ni pamoja na Uwanja wa Nachingwea unaotumiwa
na Majimaji Rangers ambao watalazimika kwenda Ilulu Lindi kucheza
mchezo wake na Mtibwa Sugar kwenye raundi hiyo.
Uwanja mwingine ni uwanja wa CCM
Mkamba Morogoro unaotumiwa na timu ya Shupavu nao hautatumika kwa
raundi hiyo na badala yake Shupavu watautumia Uwanja wa Jamhuri
Morogoro kwa mchezo wake na Azam FC.
Nayo timu ya Ihefu ya Mbarali
haitatumia Uwanja wake kwa raundi ya tatu dhidi ya Yanga na badala
yake mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine
Mbeya.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA TFF
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni