Mshambuliaji Alexis Sanchez
ataondoka Arsenal Januari iwapo itatolewa ofa nzuri na kupatikana kwa
mtu wa kuziba nafasi yake.
Ni dhahiri sasa wamiliki wa Arsenal
wameanza kuridhia kimyakimya kuondoka kwa Sanchez kwa wiki kadhaa na
sasa anaweza akaondoka baada ya kuitumikia klabu hiyo miaka mitatu na
nusu.
Hata hivyo Arsenal wanasuasua
kumuuza Sanchez bila ya kumpata mtu wa kuziba pengo lake, na kwa sasa
rada zao zinalenga kumnasa Mshambuliaji Mbrazil wa Bordeaux Malcom.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni