Kocha wa Manchester City Pep
Guardiola amesema mshambuliaji Sergio Aguero anastahili pongezi zote
baada ya kusaidia ushindi wa magoli 5-1 dhidi ya Leicester City kwa
kufunga magoli manne.
Mchezaji huyo raia wa Argentina
amefikisha magoli 13 katika michezo 10 mwaka huu akimalizia vyema
upachikaji magoli, akisaidiwa na kiwango bora cha Kevin de Bruyne,
ambaye alisaidia kupatikana magoli matatu.
Katika mchezo huo ambao Manchester
City ilipata ushindi wa 13 katika dimba la nyumbani na kuongoza kwa
tofauti ya pointi 16, ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa Raheem
Sterling, huku Jemie Vardy akiifungia Leicester goli pekee.
Raheem Sterling akiifungia Manchester City goli la kwanza katika mchezo huo
Mshambuliaji Jamie Vardy akiifungia Leicester City goli pekee katika mchezo huo
Sergio Aguero akifunga goli la pili la Manchester City na kisha baadaye kuongeza mengine matatu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni