Kocha wa Arsenal Arsene Wenger
amesema kikosi chake kinaridhika na matokeo ya kunusurika kutolewa na
timu ya ndogo ya Ostersunds FK ya Sweden na kutinga hatua ya 16 bora
katika Ligi ya Europa.
Arsenal waliokuwa wameshinda magoli
3-0 katika mchezo wa awali ilijikuta ikiduwazwa jana baada ya
kutanguliwa kufungwa magoli 2, kabla ya kurejesha goli moja kupitia
kwa Sead Kolasinac.
Wageni Ostersunds FK walipata magoli
yao kupitia kwa Hosam Aiesh na Ken Sema hata hivyo Aresenal
walijikuta wakinufaika na ushindi wa mchezo wa awali na kusonga mbe
kwa ushindi wa jumla wa magoli 4-2.
Hosam Aiesh akiachia shuti na kufunga mpira uliomshinda kipa David Ospina
Beki Sead Kolasinac akiachia shuti akifunga goli pekee la Arsenal



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni