Afisa wa polisi mmoja amekufa katika
mapigano yaliyoibuka baina ya mashabiki kabla ya mchezo wa Ligi ya
Europa baina ya wenyeji Athletic Bilbao na Spartak Moscow katika
dimba la San Mames.
Afisa huyo wa polisi kutoka
Ertzaintza wa kikosi cha polisi cha kaunti ya Basque ameripotiwa kuwa
alikufa kutokana na kupata shambulizi la moyo wakati akidhibiti
ghasia hizo za mashabiki.
Fataki na glasi zilirushwa karibu na
eneo walilikuwapo mashabiki wa Athletic Bilbao katika tukio hilo la
ghasi za mashabiki mitaani lililopelekea pia watu saba kulazwa
hospitalini.
Zaidi ya maafisa polisi 500
walipangiwa kusimamia usalama katika mchezo huo na taarifa zinasema
kuwa watu watano wamekamatwa kuhuzina na ghasia hizo.
Polisi wakimdhibiti mmoja wa mashabiki waliokuwa wakifanya fujo
Fataki zikiwa zinarushwa katika vurugu hizo mitaani zilizoibuka baina ya mashabiki wa timu hizo mbili



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni