Naibu Waziri wa Maji na
Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso akionja maji yaliyokuwa yakimwagika kutoka kwenye bomba
Naibu Waziri wa Maji na
Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso akichanganya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kisima
Naibu Waziri wa Maji na
Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso, akiwa amepanda juu ya kisima cha maji kinachojengwa
Na Mwandishi Wetu.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwangiliaji, Mheshimiwa Jumaa Aweso ameahidi serikali kupitia wizara
ya Maji kulipa kwa wakati wakandarasi waaminifu wanaosimamia miradi
ya Maji ili upatikanaji wa Maji uwe endelevu.
Mheshimiwa Aweso ameyasema hayo
Jijini Dar kwenye siku yake ya nne ya kikazi alipokuwa akikagua
maendeleo ya miradi ya Maji inayotekelezwa na Manispaa pamoja na
Miradi ya DAWASCO na DAWASA.
"Wizara ya Maji inajitahidi
kutengeneza miradi ya maji itakayomaliza tatizo la Maji kwa wananchi
hususani wananchi wenye kipato cha chini hasa vijijini, hivyo
mkandarasi atakayefanya kazi yake vizuri na kwa wakati sisi kama
serikali hatutasita kumlipa kazi yake kwa wakati"alisema Aweso



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni