Muonekano wa Nyumba yenye namba 1103/5 ambayo ipo katika eneo la Mafiat Jijini Mbeya , ilifunguliwa kesi namba 63 ya mwaka 2007 katika mahakama ya Wilaya Mbeya.
Na EmanuelMadafa,Mbeya
HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, imetoa siku saba kwa mkandarasi anayejenga nyumba ya serikali iliyoamuliwa na mahakama kuu kujengwa, kuibomoa baada ya kubainika kujengwa chini ya kiwango.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake , Afisa habari wa halmashauri hiyo, John Kilua, amesema ofisi kupitia idara ya majengo ilitembelea eneo la nyumba hiyo inayojengwa kwa amri ya mahakama kuu na kubaini changamoto mbalimbali za ujenzi.
Amesema, kutokana na changamoto hizo wahusika wanaojenga nyumba hiyo wametakiwa kuibomoa na kuanza upya kwa kufuata kanuni za ujenzi na kwamba zoezi la kubomolewa kwa jengo hilo la nyumb linatakiwa kufanyika ndani ya siku saba.
Nyumba hiyo yenye namba 1103/5 ambayo ipo katika eneo la Mafiat Jijini hapa, ilifunguliwa kesi namba 63 ya mwaka 2007 katika mahakama ya Wilaya ambayo pia ilivunja ndoa ya Mhandisi Simbonea Kileo na mkewe Gladness Kimaro na kuamuru mali za ndoa hiyo zigawanywe.
Amesema katika uamuzi huo,kileo alipeleka ombi mahakamani na kuomba nyumba hiyo isiingie kwenye mgawanyo kwa sababu aliuziwa kwa makataba maaalumu na Serikali na kwamba katika kipindi cha miaka 25 hatakiwi kuifanyia matengenezo yoyote yale ikiwamo kuiuza.
Hata hivyo aliyekuwa mke wa Kileo, mtalaka Gladness Kimaro alikata rufaa mahakama kuu kupinga ombi la mumewe ,kwa madai hakupeleka vielelezo kutoka kwa wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) kuonyesha kuwa nyumba hiyo ina mkataba maalumu na haitakiwi kuendelezwa kwa miaka 25.
Baada ya Jaji Samweli Kalua kupitia rufaa hiyo mwaka 2013, alitoa uamuzi kuwa kesi hiyo irejeshwe kwenye mahakama ya wilaya na isikilizwe na hakimu mwingine na jambo lolote lisifanyike katika nyumba hiyo.
Inadaiwa kuwa wakati Kileo akisubiri kuitwa na mahakama ya wilaya kutokana na maamuzi ya mahakama kuu, ghafla mwaka 2015 aliondolewa kwa nguvu kwenye nyumba na mtalaka wake lakini alikata rufaa.
Februari 8, 2017 Jaji Atuganile Ngwala aliagiza kesi hiyo irejeshwe mahakama ya wilaya na ipangiwe hakimu mwingine na kwamba kabla ya kesi ya msingi kusikilizwa walalamikiwa akiwemo mfanyabiashara ambaye pia ni Mbunge S.H Amoni na mtalaka wa mhandisi kileo, Gladness na madalali wawili wa mahakama kuirejesha na kuijenga upya nyumba hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni