Ndugu
waandishi wa Habari mnamo Tarehe 3 Januari 2018, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe aliteua wajumbe kumi na mbili kuunda
kamati ambayo ingetengeneza Rasimu ya katiba ya chombo cha kusimamia ngumi za
kulipwa nchini Tanzania.
Kamati
hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti ndungu Emmanuel Saleh,Joe Anea (makamu
mwenyekiti) na Yahya Poli (katibu), wajumbe wengine ni Habib Kinyogoli, Rashid
Matumla, Anthony Ruta, Shomari Kimbau, Dr. Killaga M.Killaga, Karama Nyilawila,
Fike Wilson, Jaffar Ndame na Ali C. Bakari, iliagizwa kuandaa Rasimu hiyo na
kutakiwa kuiwasilisha kwa Mheshimiwa Waziri
mnamo tarehe 31 Januari 2018, lakini kutokana na ratiba ya Mheshimiwa Waziri
kubana, kamati iliweza kumkabidhi Rasimu hiyo Tarehe 3 Februari 2018.
Baada
ya Mheshimiwa Waziri kuipokea Rasimu hiyo ya katiba ya chombo cha kusimamia Ngumi
za kulipwa nchini Tanzania, aliipongeza na kuishukuru kamati hiyo kwa kazi nzuri iliyofanya kwa umahiri mkubwa
na kujitoa kwa muda wao binafsi, na kuahidi kuwa atateua kamati nyingine na kuitangaza
Tarehe 8 Februari 2018.
Kamati
hiyo ambayo ameiteua Mheshimiwa Waziri inajumuisha wajumbe wafuatao:-
1.
Emmanuel Saleh Mwenyekiti,
2.
Joe Anea
Makamu
Mwenyekiti,
3.
Yahya Poli Katibu,
4.
Habib Kinyogoli Mjumbe,
5.
Rashid Matumla
Mjumbe,
6.
Anthony Ruta Mjumbe,
7.
Shomari Kimbau Mjumbe,
8.
Dr. Killaga M.Killaga Mjumbe,
9.
Karama Nyilawila Mjumbe,
10. Fike
Wilson Mjumbe,
11. Jaffar
Ndame
Mjumbe,
12. Ali
C. Bakari Mjumbe,
Kamati
hii itakuwa na Majukumu yafuatayo:-
- Kusaidia
Baraza la Michezo la Taifa Kuratibu shughuli za kila siku za Ngumi za
Kulipwa Nchini Tanzania.
- Kupokea
maoni kwa maandishi kutoka kwa wadau wa ngumi katika kipindi cha mwezi
mmoja kupitia tovuti ya Baraza la Michezo la Taifa ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz
na tovuti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo www.habari.go.tz
- Kuratibu
mkutano wa kujadili Rasimu katika kipindi cha miezi miwili ili kuwapa
wadau waliokosa nafasi kwa njia ya maandishi kutoa maoni yao.
- Kuandaa
mkutano mkuu wa uchaguzi.
Mwisho
kabisa kamati hii itaanza kufanya kazi leo hii Tarehe 8 Februari 2018 baada ya
kutangazwa Rasmi.
Imetolewa
na,
M.Kiganja,
Katibu
Mkuu-BMT.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni