Kocha Pep Guardiola ametwaa kombe
lake la kwanza akiinoa Manchester City baada ya kuwazidi kila idara
Arsenal na kutwaa kombe la Carabao kwa ushindi wa magoli 3-0 katika
dimba la Wembley.
City ilizinduka usingizi kutoka
kwenye kutolewa kwenye kombe la FA na timu ya ligi daraja la kwanza
Wigan Athletic, baada ya kuifundisha soka Arsenal na kuwekeza sasa
kwenye ligi kuu ya Uingereza na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mchezo huo Sergio Aguero
alikuwa wa kwanza kufunga goli baada ya beki Shkodran Mustafi kufanya
makosa, kisha baadaye Vincent Kompany akaongeza goli la pilia kabla
ya David Silva kufunga la tatu.
Sergio Aguero akifunga goli lake la kwanza kwa mpira wa kumpima urefu kipa wa Arsenal
Beki wa Manchester City Vincent Kompany akifunga goli la pili katika mchezo huo



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni