.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 26 Februari 2018

BAADA YA KICHAPO CONTE ASEMA CHELSEA INAKIBARUA KIGUMU EPL

Kocha wa Chelsea Antonio Conte amekiri kuwa haitokuwa kazi rahisi kwa kikosi chake kumaliza katika nafasi ya nne katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kufungwa magoli 2-1 na Manchester United.

Kwa matokeo hayo Chelsea imeporomoka hadi nafasi ya tato huku Tottenham ikikwea katika nafasi inayoweza kuipatia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Crystal Palace jumamosi.

Katika mchezo huo Willian alikuwa wa kwanza kufunga goli, lakini goli hilo lilisawazishwa na Romelu Lukaku na Jesse Lingard ambaye aliingia akitokea benchi akafunga goli la pili la Manchester United na kurejea katika nafasi ya pili.
   Romelu Lukaku akifunga goli la kwanza la Manchester United dhidi ya timu yake ya zamani Chelsea
 Jesse Lingard akifunga kwa kichwa goli la pili la Manchester United kwa mpira wa krosi ya Romelu Lukaku

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni