.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 19 Februari 2018

REAL MADRID YASHINDA MARCOS ANSENSIO AKITUPIA MBILI

Marco Asensio amefunga mara mbili wakati Real Madrid ikiifunga Real Betis magoli 5-3 na kupata ushindi wake wa tatu mfululizo katika La Liga.

Kikosi hicho kinachonolewa na Zinedine Zidane, kilipata goli la kuongoza wakati Asensio alipofunga goli lakini Betis wakasawazisha kupitia Aissa Mandi.

Goli la kujifunga la Nacho liliifanya Betis kuongoza lakini Sergio Ramos, Asensio na Cristiano Ronaldo wakafunga na kuifanya Real Madrid kuongeza tena.

Goli la dakika za mwisho la Sergio Leon liliibua wasiwasi na kufanya matokeo kuwa magoli 4-3 kabla ya Karim Benzema kuifungia Real goli la dakika za majeruhi.
                             Marco Asensio akishangilia baada ya kutumbukiza wavuni mpira
             Cristiano Ronaldo akijipinda na kuachia shuti lililozaa goli la nne la Real Madrid

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni