.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 20 Februari 2018

SHIDA YA MAJI JIJI LA MWANZA KUWA HISTORIA-MAJALIWA

CHANGAMOTO ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Jiji la Mwanza kuwa historia baada ya Serikali kuanza utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa miwili ya maji yenye thamani ya sh. bilioni 112.

Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Jumanne, Februari 20, 2018) wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Halmashauri za Jiji la Mwanza, Ilemela na Nyamagana akiwa katika siku ya sita ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

Waziri Mkuu amesema miradi hiyo inahusisha kuboresha upatikanaji wa maji katika maeneo ya pembezoni wenye thamani ya sh. bilioni 75 ambao utahusisha ujenzi wa chanzo kipya cha maji kwenye eneo la Butimba chenye uwezo wa kutoa lita milioni 40 kwa siku.

Ametaja maeneo yatakayonufaika na mradi huo kuwa ni Butimba, Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Sawa, Lwanhima, Kishiri, Nyahingi, Luchelele, Malimbe, Bulale, Fumagila, Usagara, Kisesa, Buswelu, Nyamwilolelwa, Kahama, Nyamadoke, Nyamhongolo, Mondo, Kiseke, Kangae, Meko, Nsumba na Bulola.

Waziri Mkuu amesema mradi mwingine ni wa kuboresha upatikanaji wa maji katika maeneo ya milimani wenye thamani ya sh. bilioni 37 ambao ulianza kutekelezwa Februari, 2017 na unatarajiwa kukamilika Agosti 2018.

Amesema wakazi 105,649 wanaoishi katika maeneo ya milimani hususan yaliyo juu ya matenki ya maji ambayo hayapati huduma kwa sasa watanufaika. Maeneo hayo ni Nyasaka, Bugarika, Nyegezi, Capripoint, Mjimwema, Nyakabungo na Kitangiri.

Amesema Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka viongozi na watendaji wa Jiji la Mwanza kuhakikisha wanashirikiana katika kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi wa dini, kabila wala kipato. Pia amewataka watambue miiko na ukomo wa madaraka yao.

Amesema watumishi hao wanatakiwa wawe waaminifu na wasimamie vizuri matumizi ya fedha za uetekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye maeneo yao na wahakikishe zinatumika katika miradi husika kama ilivyoelekezwa na Serikali.

Pia Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Bw. Kiomoni Kibamba kuifuta Taasisi ya Bunge la Jamii kwa sababu inakiuka sharia na kazi inazofanya zinalingana na za bunge. Taasisi hiyo ilisajiliwa na ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 20, 2018.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni