Timu ya Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) itacheza na Zambia katika mchezo wa kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake zitakazochezwa Ghana baadaye mwaka huu.
Twiga Stars inatakiwa kucheza mechi zote mbili kati ya April 2 na April 10,2018.
Mchezo huo ni wa raundi ya kwanza.
NGORONGORO HEROES KUCHEZA NA DR CONGO KUFUZU FAINALI ZA AFRICA
Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20(Ngorongoro Heroes) imepangwa kucheza na DR Congo kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Vijana za Africa zitakazochezwa Niger mwezi Novemba.
Mchezo wa kwanza utachezwa Tanzania kati ya Machi 30,31 na April 1,2018 na ule wa marudiano utachezwa Congo kati ya Machi 20,21 na 22.
Mshindi katika mchezo huo atacheza na Mali katika raundi ya pili itakayochezwa kati ya Mei 11,12 na 13,2018.
YANGA KUCHEZESHWA NA WAAMUZI KUTOKA BURUNDI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa(CAF) limewataja waamuzi kutoka Burundi kuwa ndio watachezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Africa kati ya Yanga ya Tanzania na Township Rollers FC ya Botswana utakaochezwa Machi 6,2018 kwenye Uwanja wa Taifa saa 10.30 jioni.
Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Willy Habimana na mwamuzi msaidizi namba mbili Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo anatoka Swaziland Mangaluso Jabulani Langwenya
Mechi ya marudiano itachezwa Machin 17,2018 nchini Botswana na itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.
Mwamuzi wa kati kati atakuwa Redouane Jiyed akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Youssef Mabrouk na mwamuzi msaidizi namba mbili Hicham Ait Abou ,mwamuzi wa akiba Samir Guezzaz na kamishna wa mchezo huo anatoka Africa Kusini Gay Makoena.
SIMBA YAPANGIWA WAAMUZI WA AFRICA KUSINI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) imewapanga waamuzi kutoka nchini Africa Kusini kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Africa Simba ya Tanzania itakapocheza na El Masry ya Misri Machi 7,2018 Uwanja wa Taifa saa 10 kamili jioni.
Mwamuzi wa kati atakuwa Thando Helpus Ndzandzeka akisaidiwa na Zakhele Thusi Siwena mwamuzi msaidizi namba moja na Athenkosi Ndongeni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Christopher Harrison na kamishna wa mchezo huo Tuccu Guish Chrbremedhin kutoka Eritrea.
Mchezo wa marudiano utachezwa huko Port Said Machi 17, 2018 utachezeshwa na waamuzi kutoka Eritrea .
Mwamuzi wa kati kati atakuwa Yonas Zekarias Ghetre akisaidiwa na Angesom Ogbamarian mwamuzi msaidizi namba moja na Yohannes Tewelde Ghebreslase mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Yemane Asfaha Gebremedhin na kamishna wa mechi hiyo anatoka Libya Gamal Salem Embaia.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni