.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 15 Februari 2018

WATUMISHI FANYENI KAZI KWA UHAKIKA NA MJIAMINI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma watumie utalaamu wao vizuri na wafanye kazi kwa uhakika na kwa kujiamini ili matokeo ya utendaji wao yaonekane.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Februari 15, 2018) mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Mwanza alipowasili mkoani hapa kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku saba.

Waziri Mkuu amesema watumishi wa umma wanatakiwa watumie utalaamu wao vizuri na wafanyekazi kwa kujiamini pamoja na kuwa na taarifa za kutosha za idara wanazoziongoza ili wananchi waweze kupata tija.

Pia amewataka watendaji kuacha urasimu na wahakikishe kila fedha iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inatumika ipasavyo.

"Msimamo wa Serikali ni kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo, hivyo watumishi wajiepushe na vitendo vya rushwa na matumizi mbaya ya fedha za umma."

Pia Waziri Mkuu amewataka watendaji hao wawe na mpango wa kuwatembelea wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili hususani za ardhi na kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongela alimueleza Waziri Mkuu kwamba atahakikisha wanafanya kazi kwa bidii na fedha zote za miradi zinatumika kama ilivyokusudiwa.

Hata hivyo Bw. Mongela alizungumza kuhusu hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika mkoa huo kuwa ni ya kuridhisha na imefikia asilimia 80, pia wameboresha huduma ya mama na mtoto.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, FEBRUARI 15, 2018.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni