Bondia Mmarekani Deontay Wilder
amesema yupo tayari kwa pambano la kuunganisha mikanda la uzito wa
juu na Muingereza Anthony Joshua baada ya kumdunda Luis Ortiz na
kutetea mkanda wake wa WBC.
Wilder, 32, alimungusha chini mara
mbili bondia raia wa Cuba Ortiz ambaye hakuwa amewahi kudundwa na
kisha kumaliaza kabisa katika raundi ya 10 katika pambano
lililofanyika Jijini New York, Marekani.
Bingwa wa mikanda ya IBF na WBA
Muingereza Anthony Joshua mwenye umri wa miaka 28, atazichapa na
bingwa wa mkanda wa WBO raia wa New Zealand, Joseph Parker huko
Cardiff tarehe 31 mwezi huu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni