Kapteni wa Fiorentina Davide Astori
amefariki dunia akiwa usingizini ikiwa ni kabla ya mchezo wao na
Udinese wa hii leo.
Astori, mwenye umri wa miaka 31 beki
wa kimataifa wa Italia amekuwa na klabu hiyo tangu mwaka 2016, hapo
awali alichezea timu za Milan, Cagliari na Roma.
Astori ameshinda makombe 14 ya
kimataifa na timu ya taifa ya Italia na alikuwa katika kikosi
kilichocheza kombe la Shirikisho la FIFA mwaka 2013.
Klabu ya Fiorentina imethibitisha kifo cha Davide Astori ambapo pia mchezo wao na Udinese umehairishwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni