Marcus Rashford amefunga magoli
mawili wakati Manchester United ikifanikiwa kuituliza Liverpool kwa
kuifunga magoli 2-1 na kuendelea kung'ang'ani katika nafasi ya pili
ya msimamo wa ligi.
Matokeo hayo yanakifanya kikosi
hicho cha Jose Mourinho kupunguza pengo na vinara wa Ligi Kuu ya
Uingereza Manchester City kuwa pointi 13 hadi hapo City itakapocheza
na Stoke jumatatu.
Rashford, ambaye alianza mchezo huo
kwa mara ya kwanza tangu Desemba 26, atapamba vichwa vya habari
lakini Romelu Lukaku ndiye alikuwa chachu ya kupatikana kwa magoli
hayo kutokana na Liverpool kushindwa kudhibiti maguvu yake.
Marcus Rashford akiangalia mpira ukielekea langoni mwa Liverpool baada ya kuachia shuti lililozaa goli la pili
Kipa David De Gea akishindwa kuzuia mpira wa goli la kujifunga uliopigwa na beki Eric Bailly
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni