Cristiano Ronaldo amefunga magoli
mawili wakati Real Madrid ikiendeleza ushindi kwa kuifunga Eibar
magoli 2-1 katika La Liga.
Katika mchezo huo wenyeji Eibar
walianza vyema lakini Ronaldo alikuwa wa kwanza kutikiza nyavu
akimalizi mpira uliopigwa na Luka Modric.
Beki wa zamani wa Wigan Ivan Ramis
alisawazisha goli hilo kwa mpira wa kichwa lakini Ronaldo tena
akafunga goli la pili kwa mpira wa kichwa.
Mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Beki Ivan Ramis akifunga goli la kusawazisha la Eibar, hata hivyo Ronaldo aliongeza la pili na kuisaidia Real kushinda
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni