Goli la dakika za ziada la Pedro
limeiwezesha Chelsea kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya
Leicester City na kutinga nusu fainali ya Kombe la FA ambapo
watavaana na Southampton katika dimba la Wembley.
Kikosi cha kocha Antonio Conte
kiligangamala katika mchezo huo baada ya kutolewa kwenye Ligi ya
Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona na kufufua matumaini ya kutwaa
kombe hilo katika msimu huu.
Katika mchezo huo Alvaro Morata
alifunga goli la kuongoza akinasa pasi ya Willian na kumfunga kipa
Kasper Schmeichel kwa utulivu, Leicester ilisawazisha goli hilo
kupitia kwa Jamie Vardy katika kipindi cha pili.
Mshambuliaji Alvaro Morata akifunga goli la kwanza la Chelsea
Pedro aliyetokea benchi akifunga goli lililoipa ushindi Chelsea



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni