Cristiano Ronaldo amefunga hat-trick
yake ya 50 katika maisha yake ya soka wakati Real Madrid ikiichakaza
Girona kwa magoli 6-3 na kukwea hadi nafasi ya tatu ya msimamo wa
ligi kuu ya Hispania La Liga.
Katika mchezo huo Cristiano Ronaldo
alifunga goli la kuongoza kutokana na krosi ya Toni Kroos lakini
Cristhian Stuani akaisawazishia Girona kwa mpira wa kichwa na kufanya
ubao kusomeka 1-1.
Ronaldo akafunga kwa shuti kali na
kumtengenezea Lucas Vazquez goli la tatu na kisha kukamilisha
hat-trick yake. Staun akaifungi Girona goli la pili naye Gareth Bale
akafunga goli la tano, Juanpe akafunga la tatu la Girona kisha
Ronaldo akafunga goli la sita.
Cristiano Ronaldo akiachia shuti na kufunga goli la kwanza katika mchezo huo
Gareth Bale aliyetokea benchi na kuingia dimbani dakika ya 70 akifunga goli



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni