Kocha wa Manchester United Jose
Mourinho amesema kwa kikosi chake kinastahili heshima baada ya
kupambana kutoka nyuma kufungwa magoli mawili na kuibuka na ushindi.
Mourinho ametoa kauli hiyo baada ya
kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya wenyeji Manchester City na
kuwachelewesha kutangazwa mabigwa wa Ligi Kuu Uingereza.
Kikosi cha United kimekuwa
kikikosolewa kwa kutokuwa na kiwango bora chini ya Mourinho, hata
hivyo matokeo hayo ya jana katika dimba la Etihad hayatosahaulika.
Mfaransa Paul Pogba akiwa ameruka juu na kupiga mpira kwa kichwa uliofanya matokeo kuwa 2-2.
Beki Chris Smalling akiachia shuti lililozaa goli la tatu na kuizamisha Manchester City katika dimba la Etihad.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni