Lionel Messi amefunga hat-trick yake
ya 40 akiwa na Barcelona na kuisaidia klabu yake katika mbio za
kuelekea kutwa ubingwa wa La Liga.
Katika mchezo huo ambao pia
Barcelona waliifikia rekodi yao ya kucheza michezo 38 ya La Liga bila
ya kufungwa Messi alifunga goli la kwanza kwa mpira wa adhabu.
Messi tena alinasa pande la Philippe
Coutinho kabla ya baadaye Lagenes kuridisha goli moja lakini Messi
tena akaongeza goli la tatu na matokeo kuwa 3-1.
Kipa wa Lagenes Cuellar akiruka bila ya mafanikio kuzuia mpira wa adhabu uliopigwa na Lionel Messi
Lionel Messi akikamilisha hat-trick katika mchezo huo baada ya kunasa pasi ya Ousmane Dembele



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni